Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Mongoloa mionongo mwa washindi tuzo ya UNEP

Rais wa Mongoloa mionongo mwa washindi tuzo ya UNEP

Rais wa Mongolia Tsakhia Elbegdorj ni miongoni mwa watu mashuhuri duniani walioshinda tuzo la kimataifa juu ya uendelezwaji wa miradi inayozingatia mustakabala wa mazingira endelevu, tuzo inayoratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP.

Wengine walioshinda tuzo hiyo ambayo inaangazia zaidi uendeshaji wa ujasilia mali wa miradi ya nishati endelevu ni pamoja na benka wa Kibrazil Fábio C. Barbosa na Dr. Sultan Ahmed Al Jaber .

Hawa ni miongoni mwa washindi wanaweka idadi jumla ya washindi sita walioshinda tuzo la mwaka huu la Umoja wa Mataifa.

Kulingana na orodha iliyotolewa na UNEP imeonyesha pia mmasaai mmoja kutoka Kenya Bwana Samson Parashina ambaye anajihusisha na miradi ya uhifadhi wa mazingira ameshinda tuzo hilo.