Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuimarisha hali ya maisha ya watu ni muhimu katika kupunguza mzigo wa Saratani- IARC

Kuimarisha hali ya maisha ya watu ni muhimu katika kupunguza mzigo wa Saratani- IARC

Utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Utafiti Kuhusu Saratani (IARC), umeonyesha kuwa kuimarisha hali ya maisha ya watu ni sehemu muhimu katika kupunguza mzigo wa saratani uliopo sasa. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ilyochapishwa leo katika jarida la Lancet Oncology.

Utafiti huo unaonyesha si tu jinsi mzigo wa saratani utayaathiri zaidi mataifa yanayofanya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, bali pia kwamba aina za saratani ambazo zinajulikana sana zinabadilika. Tayari saratani inaongoza katika kuwaua watu kwenye mataifa yenye kipato cha juu, na inatarajiwa kuwa chanzo kikubwa cha vifo katika miongo ijayo kwenye kila eneo kote ulimwenguni.