Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vyakula vilivyosahaulika vyaweza kuwa Suluhu ya Njaa:FAO

Vyakula vilivyosahaulika vyaweza kuwa Suluhu ya Njaa:FAO

Wanasayansi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa wamesema vyakula vya kiasili, ambavyo vimesahauliwa na kudhalilishwa na wakulima, viwanda vya kutengeneza chakula, pamoja na wakazi wa mijini, vinaweza kuwa sehemu muhimu ya kuepukana na njaa, lishe duni na kulinda mazingira.

Kwa muda wa karne moja, aina za mimea inayotumiwa kama chakula na matumizi mengine, imepungua tokea 100, 000 hadi 30. Wakati idadi ya watu kote duniani ikitarajiwa kupanda hadi bilioni moja ifikapo mwaka 2050, shirika la FAO lina hofu kuwa, hakutakuwa na uzalishaji wa chakula unaokidhi mahitaji ya watu hawa wengi. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)