Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuingia katika Uchumi unaojali Mazingira kunaweza Kuzalisha Ajira milioni 60:ILO/UNEP

Kuingia katika Uchumi unaojali Mazingira kunaweza Kuzalisha Ajira milioni 60:ILO/UNEP

Mabadiliko ya kuingia kwenye uchumi unaojali mazingira yanaweza kuzalisha ajira milioni 15 hadi 60 kote duniani katika miongo miwili ijayo na kuwaondoa mamilioni ya wafanyakazi katika umasikini.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya inayoongozwa na mradi wa ajira za kujali mazingira kwa ushirikiano na shirika la kazi duniani ILO na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP.

Ripoti hiyo “Juhudi za kuelekea maendeleo endelevu: fursa za ajira bora na kujumuisha jamii katika uchumi unaojali mazingira” inasema kuongeza kwa ajira hizo kutategemea endapo sera muafaka zitakuwepo. Mkurugenzi mkuu wa shirika la kazi duniani ILO Juan Somavia mfumo wa sasa umedhihirisha kwamba hautoshelezi na haufai sio tuu kwa mazingira bali pia kwa uchumi na jamii.

(SAUTI YA JUAN SOMAVIA)