Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamilioni ya Watoto wanaishi kwenye Umaskini kwenye nchi Zilizostawi:UNICEF

Mamilioni ya Watoto wanaishi kwenye Umaskini kwenye nchi Zilizostawi:UNICEF

Karibu watoto milioni 13 kwenye Jumuia ya Ulaya pamoja na mataifa ya Norway na Iceland wanaripotiwa kukosa mahitaji muhimu yanayowasaidia kukua huku watoto wengine milioni 30 kwenye nchi 35 zilizostawi kiuchumi wakiripotiwa kuishi kwenye hali ya umaskini.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa inayochunguza umaskini miongoni mwa watoto kwenye nchi zilizostawi . Gordon Alexander ni mkurugenzi wa kituo cha utafiti cha Innnocenti kilicho mjini Florence nchini Italia.

(SAUTI YA GORDON ALEXANDER)