Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mawaziri wa Afya wakutanishwa na UNAIDS na PEPFAR Kuendeleza Kupunguza Maambukizi ya Ukimwi kwa watoto

Mawaziri wa Afya wakutanishwa na UNAIDS na PEPFAR Kuendeleza Kupunguza Maambukizi ya Ukimwi kwa watoto

Mawaziri wa Afya na wawakilishi kutoka mataifa 22 ambayo yana visa vya hivi karibuni zaidi vya maambukizi ya Ukimwi  miongoni mwa watoto, wanakutana ili kutoa ripoti kuhusu juhudi zilizofanywa dhidi ya kuhakikisha hakuna maambukizi mapya ya Ukimwi miongoni mwa watoto ifikiapo mwaka 2012, na kutafuta njia za kuongeza juhudi hizo.

Mnamo mwaka wa 2010, takriban watoto 390 000 walizaliwa na virusi vya Ukimwi. Hata hivyo, kupitia njia ya huduma za kina, hatari ya maambukizi inaweza kupunguzwa kwa hadi chini ya asilimia 5. Kwa kuitikia ufahamu huu, Mpango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Ukimwi UNAIDS na Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani kwa ajili ya Ukimwi, PEPFAR, imewakutanisha wadau kubuni mpango wa kimataifa kukomesha maambukizi katika watoto ifikapo mwaka 2015, na kuzuia vifo vya akina mama. Mpango huo unaangazia mataifa 22, ambako asilimia 90 ya maambukizi mapya miongoni mwa watoto hutokea, 21 yakiwa barani Afrika. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA TAARIFA KAMILI)