Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Margaret Chan Ateuliwa tena kama Mkurugenzi Mkuu wa WHO kwa Muhula wa Pili

Margaret Chan Ateuliwa tena kama Mkurugenzi Mkuu wa WHO kwa Muhula wa Pili

Baraza Kuu la Afya Duniani, leo limemteua Bi Margaret Chan kama Mkurugezni Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO kwa muhula wa pili. Katika hotuba yake ya kukubali uteuzi huo kwa mawaziri wa afya na wawakilishi wa mataifa wanachama, Bi Chan ameahidi kuendeleza juhudi zake za kuimarisha afya ya watu wenye hali duni zaidi.

Ameongeza kuwa changamoto kubwa zaidi katika kipindi cha miaka mitano ijayo itakuwa ni kuongoza WHO katika njia zitakazoendeleza chagizo la kuhakikisha afya bora, ambalo lilianza mwanzoni mwa karne hii.