Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la G8 laafikia uamuzi kuhusu vichafuzi vya muda mfupi kwa hewa

Kundi la G8 laafikia uamuzi kuhusu vichafuzi vya muda mfupi kwa hewa

Kundi la nchi matajiri zaidi duniani la G8 wameunga mkono jitihada zenye lengo la kuondoa kile kinachofahamika kama vichafuzi vya muda mfupi kwa hewa. Utafiti unaonyesha kuwa vichafuzi vya hewa zikwemo gesi za Carbon na Methane huwa zimechangia vifo vya mapema kwa watu milioni 2.5 kila mwaka na hasara ya mamilioni ya tani za chakula. Monica Morara anaripoti.

(SAUTI YA MONICA MORARA)