Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa vikosi vya kulinda amani yuko nchini Syria kutathmini hatua zilizopigwa

Mkuu wa vikosi vya kulinda amani yuko nchini Syria kutathmini hatua zilizopigwa

Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika kitendo cha vikosi vya usalama na ulinzi wa amani Hervé Ladsous yuko nchini Syria na tayari amekutana na maafisa wa serikali na wale wa makundi ya upinzani kwa ajili ya kujadilia hali ya usalama na wakati huo huo akifanya tathmini kujua hatua zilizopigwa hadi sasa tangu kupelekwa kwa waangalizi wa kijeshi wa Umoja wa Mataifa katika maeneo yanayokumbwa na machafuko.

Mwanadiplomasia huyo aliwasili katika mji wa Homs na kufanya majadiliano kadhaa na makundi ya watu mbalimbali. Amesema wakati wa mkutano na maafisa wa serikali pamoja na makundi ya upinzani, kila upande ulielezea namna ilivyotayari kufungamana na maazimio yaliyowasilishwa na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Koff Anna anayesaka suluhu kwa pande zote.

Hata hivyo ameelezea shabaha kubwa iliyombele na kujenga dura la majadiliano na wakati huo huo kuongeza msukumo kwa pande hizo zinazohasimiana kuwa na sura ya kuaminiana.