Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu 20 huenda wamezama kwenye kisiwa cha Mayotte

Zaidi ya watu 20 huenda wamezama kwenye kisiwa cha Mayotte

Zaidi ya watu 20 huenda wamekufa au hawajulikani waliko baada ya mashua iliyokuwa imebeba karibu watu 40 ilipozama kwenye kisiwa cha Mayotte kilicho bahari ya Hindi. Miili ya watoto watatu ndiyo imepatikana hadi sasa. Kisa hiki ni ishara ya hatari wazopitia watu waofanya maamuzi ya kukimbia umaskini na mizozo nchini mwao.

Kulingana na wizara inayohusika na himaya za nje nchini Ufaransa ni kuwa watu 19 waliokolewa na kupelekwa hospitalini kwenye mji mkuu wa Mayotte Mamaoudzou. Kwa miongo kadha sasa watu wamekuwa wakitumia mashua zinazofahamika kama “kwassa- kwassa” kusafiri kutoka visiwa vya Comoro kwenda Mayotte. UNHCR imekuwa ikisadia mashirika ya umma nchini Ufaransa na himaya zake zilizo nje kukabiliana na changamoto zinazotokana na uhamiaji na wahamiaji pamoja na watafuta hifadhi.