Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Kimataifa ya Bayo-anuai:UM wahimiza ulinzi wa bahari

Siku ya Kimataifa ya Bayo-anuai:UM wahimiza ulinzi wa bahari

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema kuwa mkutano wa kimataifa ujao wa Rio+20, ni lazima uzindue mikakati ya kuimarisha udhibiti na uhifadhi wa maji ya bahari zote ulimwenguni, kupitia juhudi za pamoja- ili kuzuia uvuvi wa kupindukia, kuongeza sehemu za hifadhi ya viumbe vya majini, kupunguza uchafuzi wa maji, pamoja na ongezeko la joto duniani. Ban ameyasema haya leo, ambayo ni siku ya kimataifa ya bayo-anuai, ambayo maudhui yake hasa ni ‘bayo-anuai ya viumbe vya majini’. 

Ban ameongeza kuwa ingawa viumbe vya majini ni muhimu sana katika uhai wa binadamu, bahari kunakopatikana viumbe hivi na viumbe vyenyewe haijalindwa vyema na binadamu. Hata hivyo, amesema kuwa tayari kuna juhudi zenye kuleta matumaini ambazo zimefanywa, hasa kupitia kuweka maeneo makubwa ya hifadhi.

David Ainsworth afisa wa habari kwenye makao makuu ya ushirikiano wa bayo-anuai, Montreal, Canada, anaelezea athari za kutolinda bayo-anuai.

(CLIP YA DAVID AINSWORTH)