Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM waitoa wito wa mfumo wa kimataifa wa masuala ya kodi

Wataalamu wa UM waitoa wito wa mfumo wa kimataifa wa masuala ya kodi

Wakati mawaziri wa fedha wa mungano wa Ulaya wanakutana Mai 15, sambamba na mkutano wa mataifa nane tajiri duniani G-8 Camp David, kundi la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa wameutaka muungano wa Ulaya kushika usukani wa kuchagiza mfumo wa kimataifa wa kodi ili kukabiliana na gharama za chumi, fedha, mafuta, mabadiliko ya hali ya hewa, matatizo ya chakula na kulinda haki za msingi za binadamu.

Wataalamu hao wamesema wakati matatizo ya fedha duniani yamesababisha mamilioni ya watu kupoteza ajira, mzigo wa madeni binafsi sasa unahatarisha ukiukaji wa haki za binadamu kutokana na hatua kali za kukabiliana na matatizo ya fedha na mfumo wa fedha na kodi unaweza kuzipa serikali njia ya kulinda na kutekeleza haki za binadamu kwa watu wake. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)