Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi sahihi ya maji ni gia ya kimaendeleo-Utafiti wa UM

Matumizi sahihi ya maji ni gia ya kimaendeleo-Utafiti wa UM

Utafiti mmoja uliofanywa na Umoja wa Mataifa umebaini kuwa nchi zilizoanza kutekeleza mageuzi ya maji ziko kwenye mkondo sahihi wa kimaendeleo. Utafiti huo umesema kuwa kuwepo kwa maendeleo endelevu ya mageuzi ya maji ni hatua muhimu ambayo inachochea hatua za kimaendeleo na ukuzaji wa ustawi wa kijamii.

Utafiti huo umezingatia makubaliano ya mkutano wa kimataifa uliofanyika miaka 20 iliyopita huko Rio de Janeiro, Brazil,mkutano ambao uliweka maazimio kadhaa juu ya mazingira. Nchi ambazo tayari zimeanza kuchukua mkondo sahihi wa utekelezaji maazimio yaliyofikiwa kwenye mkutano huo zimepiga hatua kimaendeleo, imemalizia kusema utafiti huo.