Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zakubaliana kuendelea na mazungumzo kabla ya mkutano wa Rio

Nchi zakubaliana kuendelea na mazungumzo kabla ya mkutano wa Rio

Waakilishi kutoka nchi tofauti wanaojadili matokeo ya mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu wamekubaliana kuongezeka siku tano zaidi ili kuondoa tofauti zilizopo ambazo zimekuwa kizingiti cha kuendelea kwa mazungumzo hayo.

Mjadala huo na kujitolea kwa serikali, jamii za kibiasahara na mashirika ya umma unatarajiwa kutoa njia kwa watakaoshiriki kwenye mkutano wa Rio kuafikiana kabla ya mkutano huo unaong’oa nanga kuanzia tarehe 20 hadi 22 mwezi Juni mwaka huu.

Katibu mkuu wa mkutono wa Rio Sha Zukang ametaka kuwe na makubaliano pande zote akiongeza kuwa lengo kuu ni kuhakikisha kuwa yatakayojadiliwa kwenye mkutano wa Rio yako tayari.