Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wasikitikia matukio ya kuvunjwa kwa magereza Ivory Coast

UM wasikitikia matukio ya kuvunjwa kwa magereza Ivory Coast

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast UNOCI umeelezea hali ya wasiwasi kutokana na wimbi kubwa la kuvunjwa kwa magereza na umetaja shabaha yake ya kushirikiana na nchi za afrika magharibi kukabiliana na hali hiyo.

Ndani ya mwaka huu pekee ripoti zinasema kuwa magereza yanayokadiriwa kufikia tano yameripotiwa kuvunjika.

Tukio la mwisho lilitokea ijumaa iliyopita pale gereza lililopo kwenye mji mkuu Abidjan lilipovunjika. Pia hali kama hiyo imeyakumba magereza yaliyopo katika miji ya Dimbokro, Katiola, Korhogo, na Agboville.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa unaangalia uwezekano wa kushirikiana na serikali ili kuboresha hali ya usalama kwenye magereza hayo ambayo pia yanachukua idadi kubwa ya wafungwa.