Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mipango ya maendeleo endelevu lazima itekelezwa kwa pamoja kukabili tatizo la tabia nchi, yasema ESCAP

Mipango ya maendeleo endelevu lazima itekelezwa kwa pamoja kukabili tatizo la tabia nchi, yasema ESCAP

Ili kufikia ukamilifu wa kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi, basi lazima kuwekwa mikakati itayokwenda sambamba na uridhiaji ya mikataba na uwekaji msukumo dhana ya kuwa na maendeleo endelevu.

Hayo ni kwa mujibu wa afisa wa Umoja wa Mataifa anayehusika na kamshna inayoangazia masuala ya uchumi na utengamao wa kijamii kwa eneo la Asia na Pacific ESCAP.

Afisa huyo Dr. Noeleen Heyzer amesema kuwa mataifa yaliyopo kwenye eneo hilo yanapaswa kuhakikisha kwamba mipango yake yote inayotekeleza lazima iambatane na shabaha ya kuwa na maendeleo endelevu.

Amesema katika wakati ulimwengu unashuhudia majanga mengi ya kimaumbile huku mabadiliko ya tabia nchi yakiendelea kuwa suala tete, mataifa kwenye eneo hilo yanawajibika kuangazia elimu inayohusu usimamizi wa majanga.

Ametaka kuwepo kwa mashirikiano ya pamoja ili kuzikabili changamoto zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.