Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yasisitiza umuhimu wa Usafi wa Mikono

WHO yasisitiza umuhimu wa Usafi wa Mikono

Huku siku ya usafi wa mikono ikitarajiwa kuadhimishwa hapo kesho zaidi ya vituo 15,000 vya afya kutoka nchi 156,000 vinashiriki kwenye kampeni ya shirika la afya duniani WHO yenye kichwa “Okoa Maisha” kwa lengo la kutoa hamasisho kuhusu udumishaji wa usafi wakati wa kuhudumia mgonjwa.

Hii inawalenga karibu wahudumua wa afya milioni 10 katika kuhakikisha kuwepo kwa usafi wa mikono na uoshaji wa mikono mara kwa mara wanapowahudumia wagonjwa. Mengi ya magonjwa huwa yanasambazwa kwa njia ya mikono wakati wahudumu wa afya au wageni wanapowatembelea na kuwahudumia wagonjwa. Usafi wa mikono ni muhimu katika kupunguza maambukizi ya magonjwa kwa wagonjwa.