Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya kibinadamu kwenye eneo la Sahel ni mbaya:WFP

Hali ya kibinadamu kwenye eneo la Sahel ni mbaya:WFP

Ukame umerejea kwenye eneo la Sahel Afrika ya Magharibi na kuleta njaa kwa mamilioni kwa mara ya tatuu katika miaka ya hivi karibuni limesema shirika la mpango wa chakula duniani WFP.

Mkurugenzi mkuu mpya wa WFP Ertharin Cousin anaelekea kwenye eneo hilo Ijumaa ya wiki hii akiambatana na kamishina mkuu wa shirika la kuuhudumia wakimbizi UNHCR Antonio Guterres. WFP inasema kurejea haraka kwa ukame kunamaanisha kwamba watu wamekuwa na muda mfupi sana wa kujikwamua kutoka katika ukame wa awamu iliyopita.

Bei ya chakula hivi sasa iko juu sana, akiba imekwisha na mifugo mingi imetoweka. Mahitaji ya kibinadamu ni makubwa na muda wa kuchukua hatua ni sasa amesema Cosin. Ameongeza kuwa hali ni mbaya sana, na fedha za msaada hazitoshelezi sasa WFP inahitaji dola milioni 400 ili kuwasaidia watu zaidi ya milioni 8 wanaohitaji msaada Sahel.