UNHCR yaandaa mkutano kuhusu wakimbizi wa Afghanistan

30 Aprili 2012

Wakati mkutano wa kimataifa kuhusu wakimbizi wa Afghanistan utafanyika Jumatano wiki hii mjini Geneva, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudmia wakimbizi UNHCR limekwa likizungumza na wakimbizi wa Afghanistan wanaorejea nyumbani. Fida Mohamed mwenye umri wa miaka 48 alirejea nyumbani Afghanistan mwaka jana baada ya kuishi ukimbizi Pakistan kwa miaka 28.

Hivi sasa anaishi na mkewe na watoto wao wanane kwenye wilaya ya Paghman mjini Kabul, na bwana Mohamed ndio kwanza amehitimu kitado cha sita hivi karibuni baada ya kukosa fursa ya kusoma walipokimbia vamizi wa Soviet mwaka 1979. Na ameelezea maisha na ukimbizini na furaha yake ya kurejea nyumbani. Taarifa zaidi na Jason Nyakundi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter