Afisa wa masuala ya haki za binadamu wa UM kuzuru Burundi na DRC

27 Aprili 2012

Naibu mkuu wa masuala ya haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Ivan Simonovic anatarajiwa kutembelea Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuanzia tarehe 30 mwezi huu kwenye mipango ya kuboresha ushirikiano wa masuala ya haki za binadamu kati ya nchi hizo mbili .

Kwenye ziara ambayo itamchukua muda wa siku tatu nchini Burundi Simonovic atahamasisha juhudi za kubuniwa kwa tume ya uwiano na maradhiano kuambatana na viwango vya kimataifa. Akiwa kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Simonovic ataomba kuwepo ushirikiana kati ya ofisi ya mkuu wa tume ya haki za binadamu na serikali mpya. Atakapoikamilisha ziara yake Simonovic atandaa mkutano na waandishi habari kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Bujumbura nchini Burundi.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter