Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yatafuta njia ya kuwasadia watu kusoma kupitia kwa simu

UNESCO yatafuta njia ya kuwasadia watu kusoma kupitia kwa simu

Matumizi ya teknolojia ya simu za mkononi yanatajwa kurahisisha masomo ya sayanasi nchini Chile na kuboresha mawasiliano kati ya wakuu wa shule na waalimu nchini Kenya huku yakichangaia mambo mengine muhimu kwenye nchi kama vile Pakistan, barani Ulaya na nchini Argentina.

Idadi ya wanaomiliki simu za mkononi inaendelea kuongezeka hata kwenye sehemu zilizo na upungufu wa tarakilishi. Kwa sasa kuna wamiliki milioni 735 wa simu za mkononi barani Afrika. Huku kukiwa na matumizi ya juu ya simu za mkononi shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO linatafuta njia za kuwasaiadia wanaosoma, walimu na sekta yote ya elimu kwenye sehemu zilizo na viwango vya chini vya elimu.