Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO kumtangaza Sunny Varkey kuwa balozi wake wa hisani

UNESCO kumtangaza Sunny Varkey kuwa balozi wake wa hisani

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya elimu, sayansi na utamaduni UNESCO anatazamia kumtangaza Sunny Varkey ambaye ni mwelimishaji na mjasilia mali kuwa balozi wa hisani wa shirika hilo.

Bwana Varkey ambaye mwanzilishi na mwenyekiti wa shirika moja la elimu lijulikanalo GEMS anatajwa kuwa mtu muhimu hasa kutokana na mchango wake wa ubunifu uliofanikisha kuwepo kwa mashirikiano ya dhati baina ya mashirika ya umma na yale binasfi.

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na UNESCO,Bwana Varkey anatazamiwa kutangaza balozi atayehusika moja kwa moja na masula ya ushirikiano wa elimu.

Akiwa na asili ya India mtaalamu huyo alihamia Dubai mwaka 1959 ambako mwaka 1980 alianza kuiendesha shule iliyokuwa ikimilikiwa na babaake. Alifauli kuiofanikisha taasisi hiyo kutoka ya kifamilia na kuwa taasisi yenye heshima kubwa.