Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya leo ina maana kubwa katika historia ya haki na uhalifu:Wallstrom

Siku ya leo ina maana kubwa katika historia ya haki na uhalifu:Wallstrom

Kufuatia hukumu ya Charles Taylor watu mbalimbali wamekuwa wakitoa hisia zao. Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kimapenzi kwenye maeneo ya vita Margot Wallstrom amesema siku ya leo inawakilisha hatua kubwa katika historia ya kimataifa ya haki na uhalifu.

Amesema katika vita vingi makundi ya wabakaji hukwepa sheria. Wakati wa vita ukatili wa kimapenzi hujulikana kama moja ya uhalifu mkubwa unaofumbiwa macho na dunia hujivuta katika kulaani uhalifu huo.

Kesi ya Taylor Rais wa zamani wa Liberia inadhihirisha nia ya jumuiya ya kimataifa kwamba ukwepaji mkono wa sheria sio chago tena hasa kwa halifu kama huo. Kufanikiwa kumkuta na hatia kiongozi huyo wa zamani kunatoa ishara kwamba hakuna kiongozi hata awe na uwezo kiasi gani ambaye yuko juu ya sheria na kwamba hakuna mwanamke au msichana aliye chini ya sheria.