Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Charles Taylor akutwa na hatia ya kusaidia uhalifu wa vita Sierra Leone

Charles Taylor akutwa na hatia ya kusaidia uhalifu wa vita Sierra Leone

Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor amekutwa na hatia ya kusaidia na kuchochea uhalifu wa vita ikiwemo mauaji, ubakaji, na kutoa mafunzo kwa askari watoto wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone.

Taylor amebainika kuwa alikuwa akitoa msaada wa kijeshi ikiwemo silaha na mabomu kwa waasi wakati wa miaka 10 ya vita hivyo. Majaji katika mahakama maalumu ya Sierra Leone pia imekuta kwamba Rais huyo wa zamani alikuwa akipokea almasi kutoka kwa waasi kwa kubadilishana na silaha na mabomu.

Haha hivyo majaji hao wamesema kiongozi huyo wa zamani wa Liberia hakuhusika na kutoa amri ya kufanyika kwa uhalifu kwani hakuwa na mamlaka wala udhibiti wa makundi ya waasi. Jaji Richard Lussick ndiye aliyesoma hukumu hiyo.

(SAUTI YA JAJI RICHARD LUSSICK )