Ban aitaka Bahrain kuheshimu haki za msingi za binadamu

25 Aprili 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka mamlaka za Bahrain kujiweka kando na matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu na wakati huo huo amewatolea mwito viongozi wa taifa hilo kuwatendea haki raia inaoendelea kuwashikilia kwenye vizuizi.

Ripoti zinaeleza kuongezeka kwa hali ya wasiwasi hasa kufuatia kuongezeka kwa makundi ya watu wanaoandamana kwa amani wakitaka usawa wa kiraia na kuheshimiwa kwa misingi ya haki za binadamu.

Matukio hayo yanajiri katika wakati kukisubiriwa kwa mahakama kuu ya rufani kutoa uamuzi wake hapo siku ya jumatatu dhidi ya mwanaharakati mmoja ambaye alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa madai ya kuipinga serikali.

Hata hivyo mahakama hiyo sasa imesema kuwa inatazamia kutangaza maamuzi ya furani hiyo April 30. Abdulhadi Al-Khawaja alihukumiwa kwenda jela mwezi June mwaka jana, amekuwa kwenye mgomo wa kutokula.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter