Baraza la Usalama latathmini hali ya vikwazo kwa Ivory Coast

19 Aprili 2012

Pamoja na hatua kuwa za zinazoshuhudiwa sasa nchini Ivory Coast lakini hata hivyo bado kuna mikwamo ya hapa na pale inayoiandama nchi hiyo . Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa ambaye pia rais wa baraza la usalama amewaambia waandishi wa habari kuwa vikwazo vilivyowekwa kwa nchi hiyo vitaendelea kusalia kama kawaida.

Ivory Coast ilitumbukia kwenye machafuko ya kisiasa kufuatia uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka 2010 uchaguzi ambao ulishuhudia kiongozi wa upinzani akiingia madarakani.

Vikwazo kwa nchi hiyo ni vile vinavyohusu marafuku ya silaha, kutasafirisha nje kwa madini ya dhahabu pamoja na watu kadhaa wakizuiliwa kutosafiri katika nchi zozote za nje.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud