Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Migogoro duniani inawasambaratisha mamilioni ya watu, wengi Mashariki ya Kati

Migogoro duniani inawasambaratisha mamilioni ya watu, wengi Mashariki ya Kati

Wakati dunia ikijikita na watu ambao wameshindwa kukimbia ghasia Syria, ripoti mpya iliyochapishwa Alhamisi na kituo cha kuangalia wakimbizi wa ndani IDCMC imebainisha tishio linalowakabili mamilioni ya watu duniani ambao wanajikuta katikati ya hali ya kwa wakimbizi wa ndani kutokana na vita.

Watu zaidi ya milioni 3.5 walitawanywa mwaka 2011 kutokana na vita na majanga yatokanayo na hali ya hewa. Idadi hiyo ni ongezeko la asilimia 20 ikilinganishwa na mwaka 2010. Ripoti hiyo iliyoandikwa na IDCMC na baraza la wakimbizi la Norway inasema machafuko ya Afrika ya Kaskazini na Mashariki ya Kati yamewatawanya watu 830,000 mwaka 2011 ambayo ilikuwa ni mara sita zaidi ya wale waliotawanywa na katika eneo hilo mwaka mmoja kabla ya hapo.

Idadi ya waliotawanywa Afghanistan imeongezeka mara mbili, huk Somalia athari za ukame na njaa imesababisha maelfu kufungasha virago. Colombia mgene ya uhalifu na mihadarati imeendelea kushinikiza familia nyingi kukimbia nyumba zao. Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Antonio Guterres ametoa wito wa juhudi zaidi kuwasaidia wakimbizi wa ndani.

(SAUTI YA ANTONIO GUTERRES)