Pillay azitaka Sudan na Sudan Kusini kujizuia kuingia vitani

17 Aprili 2012

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amezishauri serikali za Sudan na Sudan kusini kusitisha ghasia zilizo kati yao kabla hazijahujumu makubalino ya amani yaliyo maliza vita vya miaka mingi.

Pillay amezitaka pande hizo mbili kuheshimu sheria ya kimataifa ya haki za binadamu na kuhakikisha usalama wa raia ambapo ameshutumu mashambulizi ya pande zote ambayo yamesababisha vifo vya raia. Pillay pia ameunga mkono wito wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wa kutaka kuandaliwa mkutano wa marais wa nchi hizo mbili haraka iwezekanavyo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter