Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa dunia waimarika kwa mwendo wa chini:IMF

Uchumi wa dunia waimarika kwa mwendo wa chini:IMF

Shirika la fedha duniani IMF limesema kuwa uchumi wa dunia unaimarika kwa mwendo wa chini lakini hata hivyo ukuaji huo huenda ukawa dhaifu hasa barani Ulaya huku ukosefu wa ajira ukitarajiwa kuendelea kuyakumba mataifa yaliyostawi kiuchumi.

Hata kama hatua za watunza sera barani Ulaya zimetoa mchango mkubwa bado kuna hatari ya kurudia kwa hali hiyo kwenye bara hilo. Hata hivyo kunatarajiwa kuongezeka kwa pato la taifa kati ya mwaka 2012 na 2013 huku hali ikitarajiwa kuboreka nchini Marekani. Monica Morara na taarifa kamili.

(SAUTI YA MONICA MORARA)