Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matatizo ya kisiasa Mali yanachochea ukiukwaji wa haki za binadamu:Pillay

Matatizo ya kisiasa Mali yanachochea ukiukwaji wa haki za binadamu:Pillay

Taarifa za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu zinajitokeza katika jimbo la Kaskazini mwa Mali linalodhibitiwa na waasi. Kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay amesema raia wameuawa, kuporwa, kubakwa na kulazimishwa kukimbia. Bi Pillay anasema hatari ya machafuko ya kidini inaongezeka kutokana na mvutano miongoni mwa makundi mbalimbali ya kikabila kwenye jimbo hilo.

Amesema waasi wanaodhibiti Mali Kaskazini wanahusika na baadhi ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Makundi ya wanamgambo ambayo yanazunguka katika jimbo hilo pia yanashutumiwa kwa uporaji wa mali ya umma na binafsi, ikiwepo katika hospitali na vituo vya afya. Bi Pillay ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za kitaifa na kimataifa ili kukomesha machafuko ya kisiasa nchini Mali ambayo anasema yamekuwa yakichochea ghasia na ukiukwaji wa haki za binadamu. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)