Stemp ya kuelimisha kuhusu Autism yatolewa na UM

30 Machi 2012

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya matatizo ya afya ya akili au Autism hapo Aprili pili uongozi wa huduma za posta wa Umoja wa Mataifa umetoa aina 8 za stempu ili kuelimisha umma kuhusu matatizo hayo.

Matatizo ya Autism yanaathiri maendeleo ya ubongo hasa katika Nyanja ya masuala ya kijamii na mawasiliano, na ni matatizo ambayo hayana tiba.

Nchini Marekani kiwango ya Autism kinaongezeka huku mtoto mmoja kati ya 88 wanapatwa na matatizo hayo kwa mujibu wa kitengo cha Marekani cha kudhibiti na kuzuia magonjwa.

Stemp hizo zimeundwa na watu wenye matatizo ya Autism na ziko tayari kwa ajili ya kununuliwa kupitia mtandao wa Umoja wa Mataifa wa www.unstamps.un.org

David Failor ni mkuu wa uongozi wa posta wa Umoja wa Mataifa anayehusika na stempu.

(SAUTI YA DAVID FAILOR)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter