UNAIDS na NEPAD watia sahihi makubaliano ya kupambana na ugonjwa wa Ukimwi barani Afrika

28 Machi 2012

Shirika la kupambana na ugonjwa wa ukimwi la Umoja wa Mataifa UNAIDS kwa ushirikiano na shirika la maendeleo la bara Afrika NEPAD wametia sahihi makubaliano ya kutaka   kuchukuliwa hatua zaidi katika kupambana na ugonjwa wa ukimwi barani Afrika.

Makubaliano hayo yalitiwa sahihi na mkurugenzi mkuu wa UNAIDS Michael Sidibe na mkurugenzi mkuu wa NEPAD Dr Ibrahim Mayaki mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ndizo zilizo na mzigo mzito zaidi wa tatizo la ugonjwa wa ukimwi duniani.

Mwaka 2010 asilimia 68 ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi walikuwa wakiishi kwenye nchi  zilizizo kusini mwa jangwa la sahara eneo lillilo na asilimia 12 ya watu wote duniani.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter