Wanakandanda wa kimataifa Barani Ulaya wachuana kupinga njaa Sahel:FAO

Wanakandanda wa kimataifa Barani Ulaya wachuana kupinga njaa Sahel:FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO limesema kampeni ya “wanakandanda mashuhuri kupambana na njaa” inawasili katika viwanja mbalimbali vya kabumbu barani Ulaya na ujumbe maalumu kwamba hatua zinahitajika sasa ili kuepuka janga la kibinadamu kwenye eneo la Sahel Afrika .

Eneo hilo ambako matatizo ya chakula na lishe yaliyosababishwa na ukame, umasikini uliokithiri, bei kubwa za chakula, wakimbizi wa ndani na vita yamesababisha athari kubwa kwa mamilioni ya watu.

Kampeni hiyo inachagizwa na ligi ya wataalamu wa soka Ulaya EPFL, tume ya muungano wa Ulaya na Shirika la FAO.

Mechi hizo zinaanza rasmi Machi 30 mwaka huu.

(RIPOTI YA GRACE KANEIYA)