Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya uholanzi yaachilia euoro milioni 100 za Libya

Serikali ya uholanzi yaachilia euoro milioni 100 za Libya

Serikali ya Uholanzi imeamua kuachilia baadhi ya fedha za Libya inazozizuilia na kuzitoa kwa shirika la afya duniani WHO. WHO imesema itapokea kiasi cha Euro milioni 100 kununulia madawa kwa ajili ya watu wa Libya wanaoteseka na machafuko yanayoendelea nchini mwao, na msaada huo utakwenda kwa pande zote serikalini na maeneo yanayodhibitiwa na waasi. Shirika hilo tayari linaandaa orodha ya vitu ambavyo vinahitajika haraka nchini Libya.

Kwa mujibu wa msemaji wa WHO Tarik Jasarevic awamu hii ya kwanza ya fedha itasaidia kwa takribani wiki nane na shirika hilo limesema litafanya wadau wengine kusafirisha na kusambaza msaada wa madawa.