Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya kuzorota kwa usalama yazua wasiwasi kwenye eneo la Yida, Sudan Kusini

Hali ya kuzorota kwa usalama yazua wasiwasi kwenye eneo la Yida, Sudan Kusini

Mapigano ya mara kwa mara kwenye eneo linalozozaniwa la ziwa Jau yanazua wasi wasi hasa kuhusu hatma ya wakimbizi wa Sudan walio kwenye eneo la Yida.

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa mapigano yaliripotiwa hapo jana kati ya vikosi vya serikali ya Sudan na vya Sudan Kusini kwenye ziwa Jau na sehemu zingine za mipaka.

UNHCR iko kwenye mazungumzo na viongozi wa wakimbizi iwapo itafanyika kwa haraka shughuli ya kuwahamisha raia ambao tayari wamepitia  hali ngumu.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)