Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Syria yakubaliana na mapendekezo ya mpango wa amani yaliyotolewa na Kofi Annan

Serikali ya Syria yakubaliana na mapendekezo ya mpango wa amani yaliyotolewa na Kofi Annan

 

Serikali ya Syria imemuandikia mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini humo Kofi Annan ikikubaliana na mapendekezo sita kutoka kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Annan amemuandikia rais wa Syria Bashar Al- Assad ambapo ameitaka serikali ya Syria kuyatekeleza yote kwenye majibu hayo.

Kulingana na Annan hii ni hatua nzuri ambayo itachangia katika kumaliza ghasia na umwagaji damu na kutoa mazingira mema ya kisiasa ambayo yatatoa nafasi ya kuwepo majadiliano yatakayowatimizia matarajio yao watu wa Syria. Annan ameongeza kuwa kutekelezwa kwa majibu hayo ni manufaa sio tu kwa watu wa Syria bali pia kwa wale waliojipata kwenye mzozo huo na kwa jamii ya kimataifa. Amesema baadaye leo atayaweka bayana majibu aliyopewa na serikali ya Syria

(SAUTI YA KOFI ANNAN)