Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu laitaka Syria kuheshimu wito wa wananchi wake

Baraza la haki za binadamu laitaka Syria kuheshimu wito wa wananchi wake

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limelaani vikali ukiukaji wa haki za binadamu unaondelea nchini Syria na unaoendeshwa na serikali ya Syria ukiwemo mauaji, matumizi ya nguvu kupita kiasi na mauaji ya waandamanaji, wakimbizi , watetesi wa haki za binadamu na waandishi wa habari.

 Baraza hilo limeitaka serikali ya Syria kuheshimu wito wa wananchi wa Syria na kusitisha mashambulizi na ghasia dhidi ya raia.

Mwakilishi wa Denmark kwenye Baraza la haki za binadamu alikuwa na haya ya kusema kuhusu Syria.

 (SAUTI YA MWAKILISHI WA DENMARK)