Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushahidi zaidi unahitajika kutambua ugonjwa sugu wa TB:WHO

Ushahidi zaidi unahitajika kutambua ugonjwa sugu wa TB:WHO

Wataalamu kutoka kwa shirika la afya duniani WHO wamesema kuwa kwa sasa hakuna ushahidi wa kutosha wa kuutambua ugonjwa wa kifua kikuu ulio sugu kwa madawa.

Utafiti wa madawa wa kubaini kuwa ugonjwa umekuwa sugu umekosa majibu yaliyo sahihi hasa kwa madawa yanayotumika kutibu aina ya ugonjwa wa kifua kuu ulio sugu.

Vile vile kuna kuna uwezekano kuwa madawa ambayo yanafanyiwa majaribio kwa sasa huenda yakatibu aina ya magonjwa ya kifua kikuu yaliyo sugu.

Wataalamu hao wameyataka makampuni ya kufanya utafiti pamoja na mahabara kufanya utafiti ulio wa juu ambapo pia walikubaliana kuwa WHO na washirika wengine ni lazima watoe mwongozo wa matibabu ya ugonjwa wa kifua kikuu ulio sugu, Dr Mario Raviglione ni mtaalamu wa ugonjwa wa kifua kikuu kwenye shirika la WHO.

(SAUTI YA DR. RAVIGLIONE)