UNRWA yazindua ahadi kumi kwa vijana

21 Machi 2012

Mkutano wa kimataifa wa siku mbili wenye kichwa “Kuwashirikisha Vijana: Wakimbizi wa Kipalestina katika kuibadilisha mashariki ya kati” ulioandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA umekamilika hii leo mjini Brussels  ambapo kamishina mkuu wa URWA  Filipo Grandi amezindua ahadi kumi kwa vijana kwa niaba ya UNRWA.

Mkutano huo ulihudhuriwa na washiriki 400 na washikadau wakiwemo vijana wakimbizi 24 wa kipalestina kutoka Lebanon, Jordan, Syria na eneo la wapalestina lililonyakuliwa.

Kati ya ahadi hizo ni pamoja na kufanya michango ya masomo, mafunzo kwenye nyanja mbali mbali pamoja na fursa za kufikia mashirika ya kifedha.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter