Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNECE kufanya utafiti wa kimazingira nchini Morocco

UNECE kufanya utafiti wa kimazingira nchini Morocco

Kupitia ombi la serikali ya Morocco tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi kuhusu Ulaya UNECE inatarajiwa kufanya utafiti wa kimazingira nchini humo.

Shughuli hiyo inapangwa kufanywa mwezi Septemba mwaka 2012 huku utafiti huo ukitarajiwa kukamilika mapema mwaka 2013.

Utafiti huo utafanywa kwenye nyanja 14 tofauti zilizo muhimu kwa taifa la morocco yakiwemo kwenye masuala ya utunzaji na utekelezaji wa sera na ufadhili wa miradi ya kimazingira .

Pia kati ya nyanja zitakazoshughulikiwa ni pamoja na uchafuzi wa hewa, maji, utupaji wa taka pamoja na masuala ya afya.