Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takwimu zatajwa kuwa muhimu katika kukabiliana na njaa:FAO

Takwimu zatajwa kuwa muhimu katika kukabiliana na njaa:FAO

Ufuatiliaji wa takwimu zinazohusiana na chakula pamoja na kilimo ni njia muhimu katika jitihada za kupunguza njaa na katika maendeleo.

Hii ni kulingana na kitabu cha takwimu cha kila mwaka cha shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO.

Kitabu hicho kimefanya mkusanyiko wa  takwimu kuhusu chakula na kilimo na masuala mengine yakiwemo ya kiuchumi, kimazingira na kijamii.

Baadhi ya masuala yaliyoangaziwa kwenye kitabu hicho ni pamoja na changamoto zinazokumba ardhi pamoja na maji ikiwemo uchafuzi na matumizi kupita kiasi.

Pia athari za ukosefu wa vifaa vya kilimo miongoni mwa wanawake kwa maendeleo ya kijamii na kilimo ni kati ya yale yaliyoangaziwa.