WFP kuwasaidia wanawake na watoto wenye lishe dhaifu Senegal

19 Machi 2012

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linaanza programu mpya ya kuwasaidia wanawake na watoto wenye lishe duni kwenye wilaya ya Cox’s Bazaar nchini Senegal ambako takribani asilimia 20 ya watoto wote wenye umri wa chini ya miaka 5 wana afya dhaifu na lishe duni.

Programu hiyo itatoa msaada wa lishe kwa watoto wa chini ya miaka mitano, wanawake wajawazito na wanawake wanaonyonyesha na utatoa msaada wa elimu ya lishe kwa jamii nzima.

Kwa msaada wa fedha kutoka shirika la AusAID, WFP inafanya kazi na serikali ya Senegal na  jumuiya ya masuala ya afya na maendeleo SHED ili kugawa msaada wa lishe katika vijiji vyote vya wilya ya Cox’s Bazaar, Teknaf na Ikhiya Upazilas.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter