Mwanamke wa kisomali akimbilia usalama kutokana na mapenzi yake kwa michezo

19 Machi 2012

Maymun Mahyadine alikuwa anapenda kucheza, kukimbia na pia kucheza kandanda kwenye mitaa ya mji mkuu wa Somalia Mogadishu ambapo baadaye alipata kujishindia medali na kofia.

Hata hivyo kundi la wanamgambo la Al Shabaab halikufurahishwa na tabia yake Muhyadine, lilisema kuwa  wanawake hawaruhusiwi kushiriki kwenye michezo ambapo lilimuonya akome na kuvaa hijab.

Mwaka uliopita kundi la Al Shabaab lilimuamrisha mumewe Maymun kumdhibiti mkewe agizo ambalo alilikaidi.

Hata hivyo  siku moja mumewe alivamiwa nyumbani mwao  na kundi hilo na kisha kuuawa.

Akiwa na mimba ya miezi minne Mahyadine alisubiri hadi amkamzaa mtoto Fahima kabla ya kufunga safari ndefu na ngumu kwenda nchini Djibouti.

Baada ya kuwasili nchini Djibouti Mahyadine alipata fursa ya kusafiri kwa mashua kwenda nchini Yemen fursa ambayo  hakuiitikia akihofia maisha yake.

Hata hivyo mama huyo aliweza kupata usaidizi kutoka kwa mashirika ya wakimbizi nchini Djibouti.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter