Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Annan ataka Baraza la Usalama kuwa na kauli moja dhidi ya Syria

Annan ataka Baraza la Usalama kuwa na kauli moja dhidi ya Syria

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu kwa ajili ya Syria Kofi Annan amekuwa akitoa taarifa kwenye baraza la usalama, kuhusu safari yake ya kusaka amani ya taifa hilo hivi karibuni.

Akizungumza mbele ya wandishi wa habari mjini Geneva leo Bwana Annan amesema amekuwa akilitaka baraza la usalama kuwa na kauli moja kuhusu suala la Syria, lakini amesema ni kawaida kuwa mitazamo tofauti.

Bwana Annan amesema anapeleka jumbe tena Syria kuendelea na mazungumzo na majadiliano aliyoyaanzisha.

Ameongeza kuwa atarejea Syria endapo tuu atashawishika kuwa hatua zimepigwa.

Amesema ghasia na mauaji lazima yakomeshwe na mashirika ya misaada ya kibinadamu yapewe fursa kuwafikia wanaohitaji msaada, kwani hali hiyo itahalalisha mchakato wa kisiasa unaofanyika kuelekea amani.

Amesema Syria lazima iwe makini kwani kuendelea kwa machafuko hakutakuwa janga tuu kwa Syria bali pia katika kanda nzima.

(SAUTI YA KOFI ANNAN)