Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jitihada mpya zinahitajika kumhakikishia kila mmoja maji safi

Jitihada mpya zinahitajika kumhakikishia kila mmoja maji safi

Dunia imetimiza lengo la maendeleo ya milenia la kupunguza kwa nusu idadi ya watu wasio na maji safi ya kunywa.

Njia za kuhakikisha kuwa kila moija amepata maji safi ni kati ya masuala yanayoangaziwa kwenye kongamano la sita kuhusu maji duniani linaloendelea mjini Marseille nchini Ufaransa na pia hatua zilizochukuliwa na serikali pamoja na mashirika ya umma za kuhakikisha upatikanaji wa maji safi.

Kote duniani asilimia 89 ya watu bilioni 6.1 kwa sasa wanapata maji ya kunywa ambayo ni asilimia moja zaidi ya lengo ya lengo la milenia. Hata hivyo ulimwengu uko mbali katika kutimiza usafi kama lengo la milenia na huenda lisitimizwe ifikapo mwaka 2015.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)