Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miradi ya FAO inawasaidia watunga sera kuzisaidia jamii za vijijini kuzuia matatizo ya chakula

Miradi ya FAO inawasaidia watunga sera kuzisaidia jamii za vijijini kuzuia matatizo ya chakula

Shirika la chakula na kilimo FAO limetoa nyaraka za muongozo na nyenzo za watunga sera ambazo serikali zinaweza kutumia kusaidia jamii za vijijini kufaidika na maendeleo ya nishati mbadala na kuhakikisha kwamba uzalishaji wa mazao ya nishati ya mimea haufanyiki kwa gharama za kusababisha matatizo ya chakula.

 Nyaraka hizo zilizotolewa Jumatatu na FAO ni pamoja na za njia za kutumika kutathimini athari za nishati ya mimea katika mazingira, masuala ya kichumi na kijamii.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)