Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

HRC yahofia sheria zinazokandamiza haki na kazi za waandishi habari:

HRC yahofia sheria zinazokandamiza haki na kazi za waandishi habari:

Mtaalamu wa haki za binadamu ameelezea hofu yake kuhusu kongezeka kwa serikali kutumia sheria za kuzifanya kuwa uhalifu kazi za waandishi habari na watetezi wa haki za binadamu.

Bi Margaret Sekaggya mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya watetezi wa haki za binadamu amesema amesikitishwa na ripoti ambayo inawahusisha maafisa wa serikali, majeshi ya usalama ya serikali na vyombo vya sheria katika ukiukaji wa haki za waandishi wa habari.

Amesema inasikitisha kuona kwamba kuna nchi ambazo zimepitisha sheria ambazo zinawakataza vijana wa chini ya miaka 18 au 21 kushirikia mikusanyiko ya kijamii, na kukataza matumizi ya mtandao na mifumo mingine ya mawasiliano ambayo inatumiwa na waandishi wa habari na vijana.

Katika ripoti yake kwa baraza la haki za binadamu Bi Sekaggya ameyataka mataifa kujizuia kuendelea kutumia sheria za kuwanyamazisha na kukandamiza haki za binadamu.

(SAUTI YA MARGARET SEKAGGYA)