Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yaelezea wasiwasi wake kuhusu hali nchini Syria

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yaelezea wasiwasi wake kuhusu hali nchini Syria

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema imetiwa wasi wasi kutokana na ripoti kutoka wilaya ya Baba Amro ya mji wa Homs baada ya kutwaliwa na wanajeshi wa serikali hiyo jana. Ofisi hiyo inasema kwamba haki za wale wanaozuliwa ni lazima ziheshimiwe na kuongeza uhalifu mkubwa umetendwa nchini Syria tangu mwaka uliopita.

Ofisi hiyo inautaka utawala nchini Syria kuchukua hatua za dharura kuhakikisha uhalifu huo umekomeshwa baada ya kutwaliwa kwa mji wa Baba Amro. Ripoti zinasema kuwa waasi 17 waliuawa hapo jana jinsi anavyoeleza Rupert Colville.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)