UM ni jukwaa muhimu la kujadili changamoto za dunia

2 Machi 2012

Umoja wa Mataifa ni mahala pekee paliposalia ambapo kunapatikana fursa ya kuzijadilia kwa usawa changamoto zinazoendelea kuikabili dunia wakati huu.

Akihutubu katika chuo kikuu kimoja nchini Uingereza, rais wa baraza kuu Nassir Abdulaziz Al-Nasser amesema masuala yanayohusu uchumi, siasa na mabadiliko ya teknolojia yanasalia mikononi mwa Umoja wa Mataifa.

Ameeleza kuwa hata hivyo ili kukamilisha shabaha ya Umoja huo wa Mataifa lazima kutambua umuhimu wa kukaribisha mageuzi ndani ya chombo hicho.

Amesema vyombo muhimu kwenye Umoja huo wa Mataifa kama baraza la usalama lazima litambue linapaswa kuridhia mchakato wa kufanyika mageuzi ili kwenda sambamba na changamoto zinazojiri wakati huu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter