Bahati nasibu ya anwani Uholanza na Sweden yaipa UNHCR karibu euro milioni 4:

23 Februari 2012

Bahati nasibu za anwani nchini Uholanzi na Sweden kwa mara nyingine zimetoa msaada mkubwa kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Msaada wa karibu Euro milioni 4 kwa shirika la UNHCR unajumuisha fedha kwa ajili ya kuboresha kiwango cha elimu katika kambi kubwa ya wakimbizi duniani.

Kwa kusikitishwa na hali katika kambi ya wakimbizi ya Daadab iliyoko nchini Kenya ambako kwa sasa inahifhadhi wakimbizi zaidi ya 450,000, wakati kimsingi inapaswa kuwa na wakimbizi 90,000 tu, bahati nasibu ya anwani ya Uholanzi imeamua kutoa msaada zaidi ya kawaida yake.

Bahati nasibu hiyo imetoa Euro milioni 3 zaidi kwa UNHCR ambazo zitafadhili mradi wa pamoja wa UNHCR na WFP kuboresha elimu kwenye kambi ya Dadaab. George Njogopa na maelezo kamili.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter